Kenya: Wakulima wadogo Kenya watafuta kupanua mauzo soko la China
2021-03-03 19:03:46| cri

Wakulima wadogo wa Kenya wanatafuta kupanua mauzo yao kwenye soko la China ili kufanikisha afueni ya baada ya COVID-19.

Mkuu wa muungano wa wakulima wadog Justus Lavi Mwololo amesema  kuwa masoko ya jadi ya nchi hiyo ambayo ni Marekani na Ulaya yanakabiliwa na changamoto kutokana na vizuizi vya kibiashara vilivyoletwa na janga la COVID-19 linaloendelea.

Amesema China imeweza kukabiliana na janga la COVID-19 na imefungua tena soko lake kwa uagizaji nje na hivyo ni fursa zuri kwa wakulima wa maembe, parachichi na bidhaa nyingine za kilimo.   

Mwololo ameongeza kuwa taifa hilo la Afrika mashariki limekuwa likiuza kiasi kidogo tu cha mazao yake ya kilimo nchini China lakini sasa wakulima wadogo wanapanga kuongeza.