Ujenzi wa ikolojia nchini China umepata maendeleo dhahiri katika kipindi cha Mpango wa 13 wa Maendeleo ya Miaka Mitano
2021-03-03 16:50:33| cri

Ujenzi wa ustaarabu wa ikolojia nchini China umepata maendeleo udhahiri katika kipindi cha Mpango wa 13 wa Maendeleo ya Miaka Mitano. Hatua na mafanikio ya China katika kuhimiza ujenzi wa ikolojia vimesifiwa ndani na nje ya nchi.

Katika miaka ya hivi karibuni, mji wa Shenzhen umefanya juhudi za kutafuta njia yenye maendeleo endelevu ambayo inaratibisha maendeleo ya kiuchumi, kijamii na ya mazingira, na kutimiza maendeleo yenye sifa bora ya kiuchumi na kijamii na mazingira ya ikolojia, mpango ulioonesha mafanikio mazuri katika ujenzi wa ustaarabu wa kiikolojia. Takwimu zimeonesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2019, eneo la mimea limefikia hekta laki 1 mjini Shenzhen, kiwango cha kushughulikia maji taka mjini humo kilifikia asilimia 97.71, na kile cha kushughulikia takataka za kawaida kimefikia asilimia 100. Pia bustani zaidi ya 600 zinatarajiwa kujengwa kwenye mitaa mbalimbali hadi ifikapo mwaka 2025. Mshauri mwandamizi wa Taasisi ya utafiti wa raslimali ya dunia Erik Solheim anasema:

“Mchakato wa maendeleo ya mji wa Shenzhen ni moja kati ya hadithi za mafanikio zaidi katika zama za sasa, na hakuna mji uliopata maendeleo kwa kasi kama Shenzhen. Maendeleo yake yana kiwango cha juu cha kuhifadhi mazingira, idadi ya mabasi yanayotumia nishati ya umeme imefikia elfu 16. Hii imeonesha kuwa Shenzhen imepata mabadiliko makubwa kutoka kijiji kidogo cha uvuvi kuwa mji wa kijani.”

Njia ya maendeleo endelevu ya Mji wa Shenzhen ni dirisha la kuonesha ongezeko la uwezo wa China wa kupata maendeleo endelevu wakati wa Mpango wa 13 wa Maendeleo ya Miaka Mitano. China imechukua hatua mbalimbali zenye nguvu kulinda anga, maji na ardhi safi. Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Joyce Msuya anasema:

 “Niliishi mjini Beijing tokea mwaka 2011 hadi 2014, na nilishuhudia jinsi serikali ya China ilivyofanya kazi ya uongozi katika kushughulikia takataka aina ya pm2.5. China ikiwa nchi kubwa ina anwai ya viumbe, na tumeona kuwa China imepata maendeleo makubwa na nina imani juu ya ujenzi wa ikolojia wa China.”