Kauli kuhusu China kutumia chanjo kuongeza ushawishi wake wa siasa za kijiografia ni za kupotosha
2021-03-03 19:53:49| CRI

Kauli kuhusu China kutumia chanjo kuongeza ushawishi wake wa siasa za kijiografia ni za kupotosha_fororder_微信图片_20210303194008

Msemaji wa mkutano wa 4 wa Kamati Kuu ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Bw. Guo Weimin leo amesema, kauli ya China kutumia chanjo kuongeza ushawishi wake wa siasa za kijiografia ni ya kupotosha.

Bw. Guo pia amesema, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Februari, China imetoa dozi zaidi ya milioni 52 za chanjo ya COVID-19, na nchi nyingi zimeidhinisha kutumia chanjo ya China, ikiashiria kuwa chanjo ya China ni salama na yenye ufanisi.

Amesema chanjo ni njia muhimu ya kudhibiti na kushinda janga la COVID-19, pia ni jambo muhimu kwa ushirikiano wa sasa wa wa jumuiya ya kimataifa katika mapambano dhidi ya COVID-19. Ameongeza kuwa, China imeifanya chanjo ya COVID-19 kuwa bidhaa ya umma duniani, na kujiunga kwenye mpango wa COVAX wa WHO.

Hadi kufikia mwishoni mwa Feburari, China imetoa msaada wa chanjo kwa nchi 69 na mashirika mawili ya kimataifa, na kuuza chanjo kwa nchi 28.