Kampuni kubwa ya pili ya mawasiliano ya simu nchini Zimbabwe Net One imeanzisha ushirikiano na kampuni ya Tehama ya China Huawei ili kuboresha huduma za mtandao wa kasi kwenye simu za mkononi, mradi ambao unakadiriwa kugharimu dola za kimarekani laki nne.
Maneja wa Huawei Jiang Jiaqi amesema mradi huo utakaoajiri wafanyakazi wapatao 1,500, unalenga kuimarisha usalama wa mawasiliano na kuboresha huduma zao kwenye maeneo ya mbali nchini Zimbabwe.