Sauti ya mwalimu akiwakosoa wanafunzi kutokana na mapato ya wazazi wao yazusha mjadala kwenye mtandao
2021-03-03 15:40:13| cri

Hivi karibuni sauti ya mwalimu mmoja wa kike akiwakosoa wanafunzi wake kutokana na mapato ya wazazi yao imesambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzusha mjadala mkubwa.

Katika sauti hiyo, mwalimu huyo alidai kuwa wazazi wa wanafunzi wake wa awamu zilizopita wote ni maofisa wa ngazi ya juu au wafanyabiashara matajiri, lakini wazazi wa wanafunzi wa awamu hii wote ni raia wa kawaida. Alipomkosoa mwanafunzi mmoja alisikika akisema kuwa “mapato ya mama wa XXX kwa mwaka moja yanazidi yale ya mama yako kwa miaka hamsini, kwa hiyo uwezo na sifa zenu zinawezaje kulingana? Ninyi mnawezaje kuwa sawa? Fikiria wazazi wako wana uwezo kiasi gani?”

Imefahamika kuwa mwalimu huyo wa ngazi ya kwanza wa shule ya sekondari, aliwahi kuchaguliwa kuwa “Mwalimu Bingwa” wa shule hiyo, na anapendwa sana na wanafunzi wake. Wanamtandao wanaona kauli za mwalimu huyo ni za kibaguzi, na zinaweza kutoa athari hasi za kisaikolojia kwa wanafunzi.