POOL TABLE: TAPA yaunda Kamati ya mabadiliko
2021-03-03 15:39:45| cri

Chama cha Pool Table Tanzania (TAPA) kimefanikiwa kuunda Kamati ya Mabadiliko ya kufufua na kuendeleza mchezo huo nchini humo. Kamati hiyo iliundwa katika Kikao cha wadau wa mchezo huo kilichofanyika Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa TAPA, Isack Togocho, amesema Kamati hiyo itakuwa na majukumu ya kuhakikisha mchezo huo unarejesha heshima kama awali, pia kamati hiyo itawajibika na kuongeza hamasa mchezo, kutengeneza Kamati mbalimbali za Chama, kuhamasisha uchaguzi kuanzia ngazi ya mkoa na Taifa. Togocho amesema majukumu mengine ni kuhamasisha vilabu na chama kulipa ada ya chama na Taifa na kuanzisha ligi ngazi mbalimbali.