BASKETBALL: Atalanta Hawks yamtimua Lyoyd Pierce
2021-03-03 15:38:58| cri

Timu ya Atalanata Hawks inayoshiriki Ligi ya Kikapu nchini Marekani NBA, imethibitisha kumfukuza kazi aliyekuwa kocha wake, Lyoyd Pierce kutokana na timu hiyo kufanya vibaya katika Ligi na kutoelewana kwa baadhi ya wachezaji nyota. Kocha huyo amefukuzwa baada ya kushindwa kuwasuluhisha nyota wawili wa timu hiyo, Traae Young na John Collins na hatimaye kuleta mpasuko miongoni mwa wachezaji kwenye kambi ya timu hiyo na kupelekea matokeo mabaya. Lyoyd ambaye ameiongoza Atalanta Hawks kwa muda wa misimu miwili na nusu, ameiacha timu hiyo ikiwa nafasi ya 11, wakishinda michezo 14 na kupoteza michezo 20 katika michezo 34 waliyocheza mpaka hivi sasa kwa msimu huu.