Maduka ya rejareja ya Kenya yaanza kufufuka kutoka kwenye athari za COVID-19 baada ya bidhaa kutoka China kuanza kuingia Kenya
2021-03-04 09:09:26| CRI

Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara wa rejareja ya Kenya Bibi Wambui Mbarire, amesema biashara kwenye supamaketi za Kenya imeanza kurudi katika hali ya kawaida baada ya athari za janga la COVID-19, kufuatia bidhaa kutoka China kuanza kuingia kikamilifu nchini Kenya.

Akiongea kwenye hafla ya uzinduzi wa utafiti kuhusu “Chapa 100 zinazopendwa zaidi na wanawake wa Kenya” Bibi Mbarire amesema kuingia kwa mizigo kutoka Kenya kulisimamishwa mwaka jana kutokana na hatua za zuio zilizochukuliwa na serikali ili kupambana na COVID-19. Amesema manufaa makubwa ya kuingia kwa bidhaa za China kwenye supamaketi za Kenya ni kuwapa wananchi machaguo zaidi ya kukidhi mahitaji yao.