Msaada wa chanjo ya COVID-19 kutoka China wawasili Conakry, Guinea
2021-03-04 18:24:06| CRI

Msaada wa chanjo ya COVID-19 kutoka China wawasili Conakry, Guinea_fororder___172.100.100.3_temp_9500041_1_9500041_1_1_2287d117-8680-4d25-93e0-c7344ec4b151

Msaada wa chanjo ya COVID-19 kutoka China umewasili Conakry, mji mkuu wa Guinea, na kupokelewa katika uwanja wa ndege na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Ibrahima Khalil Kaba pamoja na Balozi wa China nchini Guinea Bw. Huang Wei.

Akizungumza kwa niaba ya rais Alpha Conde wa Guinea, Bw. Kaba amemshuruku rais Xi Jinping wa China, serikali yake na wananchi wa China kwa msaada huo muhimu katika kupambana na virusi vya Corona.

Balozi Huang amesema kuwa, hiyo ni hatua mpya kwa China kutekeleza ahadi ya rais Xi Jinping ya kuifanya chanjo ya virusi vya Corona kuwa bidhaa ya umma duniani, pia ni ufafanuzi mwingine wa uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Guinea. Pia amesema anatumai kuwa chanjo hizo zitasaidia watu wa Guinea kushinda mapambano dhidi ya COVID-19 mapema.