Bei ya chai ya Uganda yaimarika katika mnada wa Mombasa
2021-03-04 19:08:24| cri

Bei ya chai imeimarika,kutoka karibu miezi miwili ya kushuka.

Haya ni kwa mujibu wa Cham cha Wafanyabishara wa Chai wa Afrika Mashariki.

Uganda na nchi nyingine wanachama huuza chai yao kupitia mnada wa Mombasa.

Bei ya chai ilishuka mwishoni mwa mwezi Januari lakini ahueni inatarajiwa kuathiri mauzo ya nje ya Uganda,ambayo yamekua yakiongezeka kwa miezi sita sasa.

Kulingana na maelezo kutoka Chama cha Wafanyabishara wa Chai Afrika Mashariki,bei ya chai iliongezeka na kufikia alama ya karibu dola mbili katika mnada wa kila wiki huku kilo moja ya chai ikiuzwa Shs7,378  kutoka Shs7,310. 

Maelezo yanaonyesha kuwa kiwango kinachotolewa kwa ajili ya kuuzwa katika mnada wa Mombasa,pia kimeongezeka huku Kenya na Uganda zikichangia sehemu kubwa zaidi.