RUGBY: Shirikisho la Raga Duniani latangaza kurejea kwa mashindano ya Raga
2021-03-04 16:01:56| cri

Shirikisho la Raga Duniani limetangaza kurejea kwa mashindano ya Raga za Dunia ya wachezaji saba kila upande kuanzia mwezi Mei 2021. Shirikisho hilo limesema jana Jumatano kuwa, mashindano hayo yataanza na duru mbili za wanawake jijini Paris nchini Ufaransa Mei 15-16 na Mei 22-23. Duru ya kwanza ya wanaume itakuwa ile ya Singapore Sevens Oktoba 29-30, ingawa inaweza kufanyika mapema kwa kuwa shirikisho hilo linazungumza na Canada na Uingereza kuona kama zinaweza kuandaa duru zao baada ya michezo ya Olimpiki itakayofanyika kati ya Julai 23 na Agosti 8 jijini Tokyo, Japan. Kenya ni moja ya mataifa yanayoshiriki duru zote za Raga za Dunia, na washiriki wengine wa raga hizo ni New Zealand, Afrika Kusini, Fiji, Amerika, Australia, Uingereza, Scotland, Wales, Ufaransa, Samoa, Uhispania, Ireland, Canada na Japan.