Rwanda yatenga dola za kimarekani milioni 51 kununua chanjo ya COVID-19
2021-03-04 16:31:35| cri

Waziri wa Afya wa Rwanda Bw. Daniel Ngamije amesema, Rwanda imetenga bajeti ya dola za kimarekani milioni 51.2 kununua chanjo ya COVID-19 kwa ajili ya watu milioni 7.8 itakapofika mwaka kesho.

Bw. Ngamije amesema, serikali itatumia zaidi ya theluthi mbili ya bajeti hiyo kununua chanjo, huku chanjo nyingine zitapatikana kutoka misaada kutoka nje na mpango wa COVAX unaoongozwa na Umoja wa Mataifa.

Habari zinasema, jana Rwanda imepokea dozi laki 2.4 za chanjo ya AstraZeneca/Oxford, na nyingine laki 1.02 za Pfizer zilipangiwa kuwasili jana usiku.