Uingereza kufadhili utafiti wa dozi ya 3 ya chanjo ya COVID-19
2021-03-04 16:33:21| cri

Serikali ya Uingereza itafadhili inachoamini kuwa utafiti wa kwanza duniani wa ufanisi wa dozi ya tatu ya chanjo ya virusi vya Corona.

Bajeti ya Uingereza imeonyesha kuwa, serikali ya nchi hiyo imetenga dola za kimarekani milioni 30.70 kwa tafiti ambazo zinajaribu ufanisi wa mchanganyiko wa chanjo mbalimbali za virusi vya Corona. Pia fedha hizo zitafadhili utafiti wa kwanza duniani utakaotathmini ufanisi wa dozi ya tatu ya chanjo ili kuboresha mwitikio wake dhidi ya virusi vya sasa vya Corona na virusi vya aina mpya vya Corona.

Dola milioni 39.07 zitawekezwa katika kuongeza uwezo wa majaribio ya chanjo nchini humo, kusaidia majaribio ya kliniki na kuboresha uwezo wa kupata sampuli haraka za aina mpya ya virusi vya Corona.