UNECA: Idadi ya waafrika wanaoishi kwenye lindi la umaskini kwa mwaka huu inaweza kuongezeka na kufikia milioni 514
2021-03-04 09:11:05| CRI

Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa mataifa UNECA, imetahadharisha kuwa janga la COVID-19 linaweza kuchochea ufakara barani Afrika wakati jumla ya watu milioni 514 wanatarajiwa kuangukia kwenye umaskini mkali mwaka huu, kama janga la hilo halitadhibitiwa.

UNECA imeonya kwenye taarifa yake kuwa janga la COVID-19 litawafanya watu kati ya milioni 5 na milioni 29 waishi chini ya kiwango cha umaskini, na kama janga halijadhibitiwa watu wengine milioni 59 watakumbwa na hali hiyo na kufanya idadi ya jumla ya watu watakaokuwa wanaishi chini ya kiwango cha umaskini kuwa milioni 514.

Makadirio ya ongezeko la uchumi na madhara ya janga la COVID-19 yanaleta mashaka kwa uwezo wa nchi za Afrika kupambana na umaskini, isipokuwa kama ongezeko la uchumi litakuwa la kasi zaidi kuliko ilivyokuwa kabla ya janga la COVID-19.