Nchi zinazozalisha mafuta zatangaza kudumisha sera za kupunguza uzalishaji
2021-03-05 17:21:32| cri

Mkutano wa 14 wa mawaziri wananchana wa Jumuiya ya Nchi Zinazozalisha Mafuta (OPEC) na zisizo wanachama umefanyika jana kwa njia ya video, na kukubaliana kuendelea kutekeleza mambo muhimu ya sera za kupunguza uzalishaji wa mafuta.

Taarifa iliyotolewa na OPEC imesema, nchi zote zimekubali kudumisha kiwango cha utengenezaji wa mafuta wa mwezi huu mpaka mwezi ujao, isipokuwa Russia na Kazakhstan. Russia imeruhusiwa kuongeza pipa laki 1.3 kwa siku na Kazakhstan kuruhusiwa kuongeza pipa elfu 20 kwa siku.

Habari zinasema, tangu mkutano wa mwezi wa Aprili mwaka jana, nchi hizo zimepunguza utengenezaji wa mafuta kwa pipa bilioni 2.3 kabla ya mwishoni mwa mwezi wa Januari mwaka huu ambapo imehimiza uwiano wa soko la mafuta.