SOKA: Simba SC yawasili Sudan kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika
2021-03-05 16:17:05| cri

Uongozi wa klabu ya Simba SC umewashukuru watanzania waliojitokeza kuwapokea mjini Khartoum, Sudan, walipokwenda kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, hatua ya makundi. Simba SC imetoa shukurani hizo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii huku ikiweka picha ya mapokezi walioyapata kutoka kwa watanzania waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum, Sudan kuwapokea. Alhamis kikosi cha kikosi cha Simba SC kitaanza mazoezi kikiwa mjini Khartoum, na kitafanya hivyo kesho kwenye uwanja Al Merrikh utakaotumika kesho. Simba SC inaongoza msimamo wa ‘Kundi A’ kwa kumiliki alama sita, baada ya kuzifunga AS Vita Club ya DR Congo na Al Ahly ya MIsri.