Mwanamke aliyempeleka mtoto wa rafiki yake shuleni kwa msaada, adaiwa fidia baada ya mtoto huyo kuumia kwa bahati mbaya
2021-03-09 11:42:25| cri

Bibi Zhang na Bibi Du kutoka mji wa Jinan, mkoani Shandong ni marafiki, na watoto wao wanasoma katika shule moja ya chekechea. Bibi Zhang ambaye hana ajira amemsaidia bila malipo Bibi Du kumpeleka mtoto shuleni na kurudi nyumbani kwa miaka miwili na nusu. Siku moja wakati akiwapeleka watoto nyumbani, kwa bahati mbaya mtoto wa Bibi Du aitwaye Jiajia alianguka kutoka kwenye kiti cha nyuma cha baiskeli ya umeme na kujeruhiwa. Baada ya kufanyiwa upimaji hospitali, mtoto huyo alilazwa hospitali kwa siku sita. Baada ya kulipwa na bima ya matibabu, matibabu yote yaligharimu yuan 7757.04, sawa na dola za kimarekani 1,200. Bibi Zhang alimpa Bibi Du yuan 2,000 alipomtembelea mtoto huyo. Baada ya tukio hilo, Bibi Du alimpeleka Bibi Zhang mahakamani, na kumtaka amlipe fidia kutokana na gharama za matibabu, uuguzi na usafiris ambazo ni yuan 6657, sawa na dola za kimarekani 1,030 kwa ujumla.

Mahakama ilitoa hukumu kuwa Bibi Zhang alipe yuan 5,000, sawa na dola za kimarekani 770, kama fidia ya kubeba watoto wawili kwa pamoja kwenye baiskeli ya umeme. Bibi Zhang alikata rufaa dhidi ya uamuzi huo. Mahakama ilitoa uamuzi ikiona Bibi Zhang aliwasaidia wazazi wa Jiajia kumtunza binti yao, na pande hizo mbili hazikufikia makubaliano ya malipo, na kuanzisha uhusiano wa msaada bila malipo. Bibi Zhang alimjeruhi Jiajia alipotoa msaada bila malipo, wazazi wa Jiajia wakiwa watu waliosaidiwa, wanatakiwa kuwajibika na fidia kwa mujibu wa sheria. Pia tabia ya Bibi Zhang ya kutoa msaada kwa majirani na marafiki ni maadili mema ambayo yanastahili kusifiwa, na kwamba kujeruhiwa kwa Jiajia kunasikitisha pande zote mbili, na wazazi wa Jiajia wanapaswa kukabiliana na tukio hilo kwa mtizamo sahihi.