Zaidi ya asilimia 80 ya wanafunzi wa shule za msingi na za sekondari hawana muda wa kutosha wa kulala
2021-03-09 11:46:14| cri

Uchunguzi uliotolewa hivi karibuni na China umeonesha kuwa, hali ya ukosefu wa usingizi kati ya vijana wa China unaendelea kuwa mbaya, na asilimia 95.5 ya wanafunzi wa shule za msingi, na muda wa usingizi wa asilimia 90.8 ya wanafunzi wa shule za sekondari na asilimia 84.1 ya wanafunzi wa sekondari ya juu haukufiki kiwango mwafaka. 

Uchunguzi huo umeonesha kuwa mwaka 2009 asilimia 47.4 ya wanafunzi walilala kwa zaidi ya saa 8 au zaidi wakati wa siku za masomo. Mwaka 2020 kiwango hicho kilipungua na kufikia asilimia 46.4.  Mwaka 2020 wastani wa usingizi wa wanafunzi ulikuwa saa 7.8, na umepungua kwa saa 0.3 kuliko mwaka 2009. 

Ripoti hiyo imependekeza kuwa, inatakiwa kuwasaidia wanafunzi kuwa na tabia nzuri ya maisha kwa lengo la kuhakikisha muda wa kutosha wa kulala na kufanya michezo, na kula mboga na matunda ya kutosha. Wakati huo huo, kuzihamasisha shule, familia na mitaa, ili kuboresha hali nzuri ya afya ya kisaikolojia ya wanafunzi.