Idadi ya wanawake wanaonunua nyumba yazidi ile ya wanaume hatua kwa hatua
2021-03-17 15:29:26| cri

Kutokana na maoni ya wachina wengi, kununua nyumba ni mahitaji ya lazima kwa wanaume wanaopanga kufunga ndoa, kwa wazazi kuwapeleka watoto kusoma shule nzuri, au kwa lengo la kuchuma pesa, na hawatarajii wanawake wenye umri wa kati ya miaka 20 na 30 ambao hawajaolewa kununua nyumba, kwani ipo siku wataolewa, na watakuwa na faida gani ya kununua nyumba?

Lakini kutokana na takwimu mbalimbali, katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya wanawake wanaonunua nyumba imezidi ile ya wanaume hatua kwa hatua, haswa baada ya mwaka 2018, idadi ya wanawake wanaonunua nyumba imezidi asilimia 50, na kuzidi kuongezeka mwaka hadi mwaka. Mjini Shenzhen, idadi hiyo imefikia asilimia 53.3 kati ya idadi ya jumla ya watu walionunua nyumba mwaka jana.

Baadhi ya watu wanaona hali hii imeonesha wanawake kujitegemea kiuchumi. Lakini kununua nyumba sio jambo rahisi. Ni msukumo gani unaowafanya wanawake kupendelea kununua nyumba wanapobana matumizi ya fedha kwa nguvu? Ikiwa unataka kuuliza maoni ya wanawake ambao wamenunua nyumba, walionunua wanasema sio kwamba wamenunua nyumba tu, bali ni kujiweka salama.