Matumizi ya fedha ya wanawake kwa lengo la kujiburudisha yamekuwa mwenendo mpya wa matumizi ya wanawake katika China Bara
2021-03-17 15:30:30| cri

Janga la virusi vya Corona linalowalazimisha watu kukaa nyumbani, liliwahimiza wanawake kufanya matumizi ya fedha zaidi kwaajili ya kujiburudisha, na pia kuwa mwenendo mpya wa matumizi wa wanawake katika China Bara.

Ripoti kuhusu Mwelekeo mpya wa matumzi ya wanawake katika China Bara ya mwaka 2020 iliyotolewa hivi karibuni imeonesha kuwa, matumizi yanayohusiana na janga la virusi vya Corona yalifufuka kwa kiasi kikubwa ndani ya muda mfupi. Matumizi katika bidhaa za vipodozi, utunzaji wa watoto, na usimamizi wa afya yalikua kwa haraka.

Ripoti hiyo pia imeonesha kuwa, matumizi ya fedha katika chesi, mahjong, na kaligrafia yaliongezeka kwa 70%, na 54% mtawalia; matumizi ya fedha ya wanawake katika utunzaji wa mwili na uso yaliongezeka kwa 117% na 66% mtawalia, na matumizi kati ya wanawake wenye umri wa miaka 46 na 55 yaliongezeka kwa asilimia 33.8.