Idadi ya ndoa zilizosajiliwa mwaka 2020 nchini China yashuka kwa asilimia 12.2
2021-03-17 15:31:09| cri

Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Wizara ya Mambo ya Kiraia ya China zinaonesha kuwa idadi ya ndoa zilizosajiliwa mwaka 2020 ilipungua kwa asilimia 12.2 kuliko mwaka juzi, ukiwa ni mwaka wa saba mfululizo kiwango hicho kuendelea kushuka.

Kupungua huko katika mwaka 2020 kunatokana na sababu mbalimbali, ikwa ni pamoja na kufungwa kwa muda mrefu kwa ofisi za usajili wa ndoa kote nchini kutokana na janga la Corona, kupungua kwa idadi ya watu wenye umri wa kufunga ndoa, kuongezeka kwa umri wa wastani wa kufunga ndoa na kuongezeka kwa watu waliochelewa kufunga ndoa na wasiotaka kufunga ndoa.

Aidha, bei kubwa ya nyumba katika miji mikubwa na shinikzo kubwa la kichumi pia vimechangia kupungua huko.

Katika miaka ya karibuni, kupungua kwa idadi ya ndoa zilizosajiliwa na kushuka kwa kiwango cha uzazi vimezusha mjadala katika jamii. Moja ya sababu ni kuwa wanadoa wengi hawana nia ya kupata mtoto, baadhi ya wanawake wenye umri unaofaa kuzaa hawataki kuzaa kutokana na gharama kubwa za muda na fedha katika kuzaa na kulea mtoto.