Vituo vya Subway mjini Beijing vyaboresha utoaji wa huduma
2021-03-17 15:28:44| cri

Vituo vya Subway havitakuwa tu mahali pa kupanda treni, bali pia vitakuwa nafasi ya kutoa burudani kwa wananchi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Kazi ya Usafiri wa Beijing mwaka huu, vituo vidogo 71 vya burudani vitajengwa karibu na vituo vya Subway mjini Beijing, ili kuunganisha mfumo wa usafirishaji na maendeleo ya miji. Wakati huo huo, baadhi ya vituo vya subway vitajaribu mfumo mpya wa kupima usalama kwa mujibu wa hali ya imani ya abiria ili kuwawezesha waingie vituoni kwa haraka.

 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Beijing pia itazidi kuboresha vituo vya utoaji wa huduma kwenye vituo vya Subway, kama vile kuanzisha maduka . Naibu mkurugenzi wa Ofisi ya utafiti kwenye Kamati ya Usafiri ya Beijing Bw. Feng Tao ameeleza kuwa, vituo vya Subway havitakuwa mahali ambapo abiria wanapita kwa haraka, bali pia vitakuwa vituo vyenye uhai vya mji.