Kijana apewa likizo ya siku 16 kutokana na kupanda miti kupitia App ya Alipay
2021-03-17 15:29:54| cri

Hivi karibuni kijana mmoja kutoka mji wa Xi’an alifanikiwa kupata likizo ya siku 16 kutokana maksi alizopata za kupanda miti kupitia App ya Alipay.

Meneja wa kampuni ya vifaa vya michezo anayofanya kazi kijana huyo amesema, kampuni yake imetoa likizo hiyo kama zawadi kwa wafanyakazi wake ili kuwahamasisha washiriki zaidi kwenye mazoezi ya viungo na kutumia zaidi usafiri usioleta uchafuzi.

Kabla ya hapo mjini Wuhan mkoani Hubei, kampuni nyingine ilitoa zawadi ya “Koponi ya kufika mapema” kwa wafanyakazi wake waliowasili ofisini mapema, ili kutatua suala la wafanyakazi kuchelewa kufika kazini.

Koponi hizo zinaweza kutumika kwa njia mbalimbali, ikiwemo kusamehe muda wa kufika kazini, kubadilisha zamu au kupata kahawa bure ya Starbucks.