Wataalamu wasema kuongeza umri wa kustaafu hakuzuii fursa za ajira kwa vijana
2021-03-22 14:31:56| cri

Hivi karibuni mpango wa kuongeza umri wa kustaafu umezusha mjadala mkubwa kwenye jamii.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Idara kuu ya takwimu ya China, mwishoni mwa mwaka 2019, idadi ya wazee wenye umri zaidi ya miaka 60 nchini China ilifikia milioni 254, ikiwa ni asilimia 18.1 ya jumla ya watu wa China, huku idadi ya wazee wenye umri zaidi ya miaka 65 ikifikia milioni 176, ikiwa ni asilimia 12.6 ya jumla ya watu. Inakadiriwa kuwa katika mpango wa 14 wa maendeleo ya miaka mitano, idadi ya wazee nchini China itazidi milioni 300, na kuifanya China iingie kwenye kipindi chenye wazee wengi.

Naibu mkuu wa Chuo cha utafiti wa bima katika Chuo kikuu cha Uchumi na Biashara ya Kimataifa Sun Jie amesema kimsingi sera ya kuongeza umri wa kustaafu haitaleta athari hasi kwa mapato ya mtu binafsi. Amesema mapato ya ziada watakayopata baada ya umri wa kustaafu kuongezwa, yatazidi kwa kiasi kikubwa malipo ya bima ya kijamii katika miaka ya kazi itakayoongezwa. Kwa hivyo sera hiyo itasaidia kuboresha hali ya kiuchumi kwa mfanyakazi binafsi na familia yake.