Rais wa China ampongeza rais mpya wa Tanzania
2021-03-25 19:44:04| CRI

Rais wa China ampongeza rais mpya wa Tanzania_fororder_VCG111322001536

Rais Xi Jinping wa China leo amemwandikia barua ya pongezi rais mpya wa Tanzania Bibi Samia Suluhu Hassan.

Katika barua hiyo, rais Xi amesema, urafiki wa jadi kati ya China na Tanzania ni mkubwa, na ushirikiano wa sekta mbalibmali umepata matoko makubwa. Amesema China inazingatia sana maendeleo ya uhusiano kati yake na Tanzania, na anapenda kushirikiana na rais Samia kuhimiza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa pande zote wa kunufaishana kati ya China na Tanzania kupata maendeleo mapya, na kunufaisha nchi hizo mbili na watu wao.