Mwanamume mmoja atengeneza mavazi kwa kutumia mfuko wa plastiki wa kubebea mbolea
2021-03-30 21:05:40| cri

Bw. Zhong kutoka mji wa Yibin, mkoani Sichuan, anaendesha duka moja la nguo. Mtindo wa nguo za duka lake unapendeza, na haikuchukua muda mrefu kwa nguo zote kwisha dukani. Siku moja aligundua kuwa mfuko wa plastiki wa kubebea mbolea ya Urea una rangi ng’aavu, na alitarajia kuwa nguo zikitengenezwa kwa mfuko wa aina hiyo zitaonekana vizuri. Hapo awali alifanya majaribio tu lakini hakutarajia kama zitajulikana kupitia mtandao wa Internet.

Katika picha zilizosambazwa kupitia mtandao wa Internet, nguo zilizotengenezwa kwa mifuko ya Urea zimetundikwa dukani, na rangi za nguo hizo ni zinapendeza sana chini ya mwanga wa taa. Baadhi ya watu wanaona ajabu kuwa, Bw. Zhong anaendesha duka la nguo, kwa nini alifikiria kutengeneza nguo. 

Akijibu swali hilo Bw. Zhong alisema ingawa ana duka la nguo, lakini pia anapenda kutengeneza nguo. Alifanya hivyo kwa kujiburudisha, lakini hakutarajia kuwa watu wengi watazipenda. Pia amesema nguo za aina hii zinatengenezwa kwa mikono, na anaweza kutengeneza moja tu kwa siku, na bei ya sasa ni yuan 300, sawa na dola za kimarekani 45.

Lakini wanamtandao wengine wanaona ingawa mtindo huu wa mavazi unaonekana vizuri, lakini watu hawataona faraja kuzivaa.