China yapitisha kiambatisho cha kwanza na cha pili cha Sheria ya kimsingi ya Hong Kong
2021-03-30 19:53:46| CRI

China yapitisha kiambatisho cha kwanza na cha pili cha Sheria ya kimsingi ya Hong Kong_fororder_VCG111173487850

Mkutano wa 27 wa Kamati ya kudumu ya bunge la 13 la umma la China umefungwa leo hapa Beijing, ambapo umepitisha kiambatisho cha kwanza cha Sheria ya kimsingi ya Hong Kong, njia ya kuteua mtendaji mkuu wa mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong, na kiambatisho cha pili cha Sheria ya kimsingi ya Hong Kong, njia ya kuchagua wajumbe wa baraza la kutunga sheria na mchakato wa kupitisha sheria wa baraza hilo.

Wizara ya mambo ya nje ya China leo imetoa taarifa ikisema kupitishwa kwa viambatisho hivi viwili na kurekebisha na kukamilisha njia ya kuteua mtendaji mkuu na wajumbe wa baraza la kutunga sheria la Hong Kong, kutatoa uhakikisho wa mfumo wa kutekeleza kanuni ya “Nchi Moja, Mifumo Miwili”, kanuni ya “Wahongkong kuitawala Hong Kong” na kuhakikisha usalama wa kudumu wa Hong Kong, pia kumeonyesha vya kutosha nia ya pamoja ya wananchi wa China wakiwemo ndugu wa Hong Kong.