Watu wanne wauawa kwa kupigwa risasi kaunti ya Orange, jimboni California, Marekani
2021-04-02 09:08:37| CRI

Polisi nchini Marekani wamesema tukio la ufyatuaji risasi lililotokea Jumatano jioni katika kaunti ya Orange, kusini mwa jimbo la California, limesababisha vifo vya watu wanne, akiwemo mtoto mmoja, na wengine wawili kujeruhiwa.

Polisi wamemkamata mshukiwa, na uchunguzi unaendelea kuhusiana na tukio hilo.