Mamlaka ya mfereji wa Suez yadai fidia ya zaidi ya dola za kimarekani bilioni moja kutokana na kukwama kwa meli ya “Ever Given”
2021-04-02 09:07:18| CRI

Mamlaka ya mfereji wa Suez imedai fidia ya dola za kimarekani bilioni moja kutokana na meli kubwa ya mizigo ya “Ever Given” kukwama na kuziba mfereji huo kwa siku sita.

Mwenyekiti wa mamlaka hiyo Osama Rabie amesema, ajali hiyo imeleta hasara ya dola za kimarekani milioni 14 hadi milioni 15 kwa siku. Meli ya Ever Given ambayo imetia nanga katika ziwa Great Bitter haitaruhusiwa kuondoka kabla ya kumalizika kwa uchunguzi na kufikiwa kwa makubaliano ya fidia.