Russia yasema inachukua hatua za lazima kuhakikisha usalama wa mpaka wake
2021-04-02 09:08:10| CRI

Msemaji wa Ikulu ya Russia (Kremlin), Dmitry Peskov amesema nguvu za kijeshi za nchi za NATO na pande nyingine zinazidi kuongezeka kwenye maeneo ya mpaka wa Russia, hali ambayo imeilazimisha Russia ichukue tahadhari. Amesema Russia inachukua hatua za lazima kulinda usalama wa mpaka wake.

Msemaji huyo amesema, jeshi la Russia halikuwahi kushiriki kwenye mapambano ya ndani ya Ukraine, na kwamba Russia, nchi za Ulaya na nchi nyingine duniani zote hazitaki vita irudi tena nchini Ukraine.