Wafungwa wasiopungua 90 watoroka jela Liberia
2021-04-02 09:07:49| CRI

Polisi nchini Liberia wamethibitisha kuwa wafungwa wasiopungua 90 wametoroka kwenye gereza lililoko kaunti ya Maryland, kusini mashariki mwa nchi hiyo, baada ya waandamanaji kuvamia na kuchoma moto gereza hilo.

Serikali ya Liberia imetangaza marufuku ya kutotembea usiku katika kaunti ya Maryland kuanzia jana Alhamisi.