Wakazi Kuhamishiwa kwingine kutokana na dhahabu
2021-04-02 16:47:51| CRI

Asilimia 80 ya wakazi wa kaunti za Pwani nchini Kenya wanatarajiwa kuhamishiwa bara baada ya kugunduliwa kwa kiasi kikubwa zaidi cha dhahabu katika maeneo wanayokaa.

Kulingana na kampuni ya Kenya Coast Gold Exploration and Mining Inc, kaunti ambazo zaidi ya wakazi wake asilimia 80 watahamishwa ni Kilifi, Kwale, Lamu na Mombasa.

Wakazi hao watahamishiwa kaunti za Turkana, Marsabit, Mandera, Wajir, Garissa, Kiambu, Nyeri na Kisii

Mkuu wa kampuni hiyo Bw Niklas Saizler amesema mbali na kuwahamisha pia watawajengea wakazi hao hospitali, shule, stima, maji na barabara za kisasa katika makazi hayo mapya.

Kampuni hiyo imekuwa ikifanya utafiti eneo hilo la Pwani ya Kenya kwa muda mrefu na hatimaye imethibitisha kuna dhahabu nyingi na ya thamani kubwa. Kiasi kikubwa zaidi cha dhahabu kinapatikana katika kaunti ya Lamu chini ya bahari. Dhahabu hiyo ni ya ubora wa juu kuliko nyingine yoyote duniani.

Alisema mpango huo wa kuhamisha wakazi utaanza kutekelezwa baada ya kushauriana na viongozi wa eneo hilo na kukubaliana kuhusu fidia inayopasa kulipwa wakazi.