Wachezaji wa AC MILAN kupata magari ya BWM wanayotaka baada ya mkataba
2021-04-02 16:32:11| CRI

Wachezaji wa AC Milan sasa wana nafasi ya kwenda kwenye ofisi za kampuni maarufu ya magari ya kifahari ya BMW kujichagulia magari wanayotaka baada ya klabu yao kuingia mkataba na watengenezaji magari hayo. Mshambuliaji mkongwe, Zlatan Ibrahimovic ataongoza wachezaji wenzake wa klabu hiyo ya Italia kwenda kujichagulia magari ambayo "roho yao" inapenda baada ya mkataba huo kusainiwa jana Jumatano. BMW imekuwa mshirika mpya wa magari wa AC Milan na makubaliano ya udhamini huo yanaitaka BMW kuwapa wachezaji magari watakayopenda. Makubaliano hayo yanaonesha kuwa mikataba kati ya klabu na wachezaji inaweza kuwa na manufaa makubwa kwa wachezaji, na sio kwa makampuni tu.