Klabu ya Namungo FC yasema hairudii makosa ya huko nyuma
2021-04-02 16:32:39| CRI

Klabu ya Namungo FC ipo katika maandalizi ya mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa nchini kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam dhidi ya Nkana Red Devils Zambia kesho. Namungo ilianza kwa kusuasua hatua ya makundi ya michuano hiyo baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo ya awali ugenini dhidi ya Raja Cassablanca ya Morocco na nyumbani dhidi ya Al Masry ya Misri, hivyo kujiweka katika mazingira magumu. Kocha mkuu wa timu hiyo, Hemed Moroco amesema wachezaji wana morali wa juu na maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kilichobaki ni sapoti kutoka kwa mashabiki wao.