Kocha wa AS VITA matatani baada ta DRC kutolewa AFCON, anafikiria kumalizia hasira Simba
2021-04-02 16:31:36| CRI

Frolent Ibenge, Kocha Mkuu wa Klabu ya AS Vita ambaye pia anainoa timu ya taifa ya DR Congo amekumbwa na changamoto kubwa  baada ya timu yake ya taifa kufungashiwa virago kwenye michezo ya kuwania kufuzu kombe la mataifa ya Afrika (AFCON). Hali hiyo inamfanya awe na shinikizo zaidi kwenye mechi ya kesho dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi. Ibenge amesema ratiba za maandalizi zimekuwa ngumu jambo ambalo linampa kazi kubwa ya kufanya ila anaamini kwamba watafanya vizuri kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba. Habari nyingine kuhusu mechi hiyo zinasema kuwa mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema baada ya kuruhusiwa kuingiza mshabiki kwenye mchezo huo. Ruksa hiyo imekuja kufuatia katazo lililowekwa mara ya kwanza kwa klabu hiyo kutocheza bila mashabiki kwenye mchezo wao wa marudiano dhidi ya Al Merreikh ya Sudan uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam. Lakini sasa CAF imeruhusu mashabiki 10,000 katika dhidi ya AS Vita.