Kibarua cha Kocha Molefi Ntseki wa Bafana Bafana ya Afrika Kusini chaota mbawa
2021-04-02 16:30:59| CRI

Kocha Molefi Ntseki wa timu ya taifa ya Afrika Kusini Bafana Bafana, amefutwa kazi baada ya kushindwa kuongoza kikosi chake kufuzu kwa fainali za Kombe la Afrika (AFCON) 2022 nchini Cameroon. Kutimuliwa kwa Ntseki kulichochewa na matokeo duni ya Bafana Bafana katika mechi mbili za mwisho za makundi ambapo waliambulia sare ya 1-1 dhidi ya Ghana nyumbani kisha wakazidiwa maarifa na Sudan kwa kichapo cha 2-0 ugenini. Baada ya kukabwa koo na Ghana, Bafana Bafana walikuwa wanahitaji sare ya aina yoyote dhidi ya Sudan ili kujikatia tiketi ya kuelekea Cameroon mnamo Januari 2022. Ntseki amekiri kwamba kutofuzu kwa Afrika Kusini kwenye fainali za AFCON kulikuwa kumesfanya  watu wengi wa taifa hilo kuwa na machungu .