RIADHA: Ruth Chepngetich avunja rekodi ya dunia Istanbul
2021-04-05 16:43:10| cri

Mwanariadha wa Kenya Ruth Chepng'etich ameweka historia baada ya kuvunja rekodi ya dunia katika mbio za kilomita 21 za Istanbul Half Marathon. Chepng'etich alitumia muda wa saa 1:04:02 kushinda mbio hizo jana Jumapili, na kuweka rekodi mpya. Bingwa huyo wa dunia mbio za marathon alikuwa sambamba na mwanariadha mwingine wa Kenya Hellen Obiri na Muethiopia, Yalemzerf Yehualaw kabla ya kupenya kupata ushindi. Hii ni mara ya tatu Ruth Chepng'etich kushinda mbio hizo baada ya kuibuka mshindi mwaka 2017 na 2019. Kwa upande wa wanaume, Mkenya Kibiwott Kandie aliibuka mshindi na rekodi ya 59:35 na kumshinda Mkenya mwenzake Geoffrey Kamworor.