IMF YAIPA SUDAN KUSINI $174M KUKABILIANA NA ATHARI ZA CORONA.
2021-04-05 18:15:06| cri

 

Mwishoni wa wiki jana, bodi ya shirika la fedha la kimataifa (IMF), liliidhinisha utoaji wa dola milioni 174.2 kwa taifa la Sudan kusini, ili kulisaidia katika kukabiliana na makali ya virusi vya corona kwa uchumi wake kitaifa.

Bodi ya IMF iliidhinisha fedha hizo, huu ukiwa ni msaada wa pili kutoka kwa shirika hilo kwa Sudan kusini, tangu taifa hili lijiunge na shirika hilo mwaka wa 2012.

Fedha hizi zitasaidia sana Sudan Kusini kujikwamua kiuchumi huku ikijaribu kuongeza kasi ya kupunguza umaskini. Taifa hili limeathirika mno kutokana na kushuka kwa bei za mafuta kimataifa. Aidha, mafuriko yaliyoshuhudiwa nchini humo, yaliathiri hatua za kiuchumi zilizokuwa zimepigwa na kusababisha uchumi kushuka kwa asilimia 4.2 mwaka wa fedha wa 2020/21.