SULUHU AZIMA NYONGEZA YA USHURU
2021-04-05 18:13:24| cri

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameionya Mamlaka ya Ushuru (TRA), dhidi ya kupandisha ushuru. Rais Suluhu alisema mtindo huo ni wa kunyanyasa wafanyabiashara na raia, na badala yake akataka TRA itafute mbinu nyingine za kuongeza mapato ya nchi. Kulingana na rais huyo, TRA imekuwa ikiwakandamiza wafanyibiashara wengi n ahata kuwalazimu wengi kufunga biashara zao nchini Tanzania, na kwenda kufanya biasharam hizo katika mataifa mengine. Alisisitiza kuwa TRA inapewa shilingi trilioni 2 kwa mwezi, na wanapswa kuja na mbinu mwafaka za kukusanya mapato, bila kuwadhulumu wananchi.

Rais huyo alikuwa akizungumza kwenye hafla ya kuapishwa kwa katibu mpya wa Utumishi wa Umma, mawaziri na manaibu wao katika Ikulu ya Dodoma

.Kulingana na rais huyo, mtindo wa sasa unaua biashara badala ya kuimarisha mazingira ya kufanya biashara. Awali, Makamu wa Rais Dkt Phillip Mpango ambaye pia alihutubu alisema bado kuna kazi nyingi ya kufanya katika ukusanyaji wa mapato na matumizi ya pesa za umma hasa katika serikali za wilaya.