KENYA KUDHIBITI UVAMIZI WA NZIGE WA JANGWANI
2021-04-05 18:14:00| cri

 

Kenya imetangaza kuwa uvamizi wa nzige wa jangwani utadhibitiwa kikamilifu ifikapo katikati ya mwezi huu.

Akiongea na wanahabari mjini Nairobi, msemaji wa serikali Cyrus Oguna amesema juhudi za kudhibiti na kuzuia nzige hao zinafanywa na serikali kuu ikishirikiana na serikali za kaunti pamoja na washirika wengine wa kimaendeleo.

Alisema upambanaji wa nzige hao unausaidizi mkubwa kutoka shirika la shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, Shirika la Kudhibiti Nzige wa Jangwani la Afrika Mashariki DLCEO na Benki ya Dunia.

Juhudi zilizochukuliwa hadi sasa katika kukabiliana na nzige zimezaa matunda ambapo zimepunguza makundi ya nzige hadi matatu na kusisitiza kwamba juhudi zinaendelea kufanywa ili kudhibiti kundi la mwisho.

Oguna alibainisha kuwa jumla ya kaunti 25 zimevamiwa na wadudu hao kwa kiwango tofauti na sasa kuna maendeleo makubwa yaliyofikiwa ya kuwadhibiti.