SOKA: Vilabu vya Tanzania vina pesa asema Ibenge
2021-04-05 16:42:47| cri

Kocha wa timu ya AS Vita ya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Florent Ibenge amekiri kuwa kwa sasa vilabu vya Tanzania vimeimarika kifedha hovyo kuwa na uwezo wa kusajili wachezaji kwenye vilabu vikubwa kama TP Mazembe na AS Vita vya nchini DRC. Kauli hiyo ameitoa baada ya timu hizo za DRC kuondolewa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku Simba SC ya Tanzania ikifuzu robo fainali kwa kuongoza kundi A. Simba imefuzu robo fainali baada ya jumamosi kuifunga AS Vita magoli 4-1 na kufikisha pointi 13 na kuongoza Kundi A lenye timu za Al Ahly, AS Vita na Al-Merrikh.