SOKA: Timu ya Polisi Tanzania yasimamisha watano
2021-04-05 16:43:29| cri

Uongozi wa timu ya Polisi Tanzania, umetangaza kuwasimamisha wachezaji watano kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu. Taarifa rasmi iliyotolewa jumamozi na Ofisa Habari na Mawasiliano wa Polisi Tanzania, Hassan Juma, imebainisha wazi kwamba, nyota hao wamesimamishwa kutokana na tabia hiyo kuota mizizi licha ya kupelekwa mara kadhaa kwenye kamati ya nidhamu. Nyota waliosimamishwa ni Pius Buswita, Rashid Juma, Abdulaziz Makame, Tariq Seif, George Mpole na Abdulmalick Adam. Taarifa hiyo ilifafanua zaidi kwa kusema Rashid amesimamishwa kutokana na kutofika kambini tangu Februari 29 alipotakiwa arudi baada ya kuomba ruhusa ya kuhudhuria harusi ya kaka yake, huku Mpole akitoroka kambini wakati kikosi hicho kilipoenda Mwanza kucheza na Gwambina FC.