Uganda yawaokoa wasichana 29 wa Burundi na kuwakamata washukiwa watano wa biashara ya kusafirisha binadamu
2021-04-06 19:30:40| Cri

Polisi nchini Uganda imewaokoa wasichana 29 wa Burundi na kuwakamata watu watano wanaoshukiwa kuhusika na biashara haramu ya kusafirisha binadamu nchini humo.

Msemaji wa jeshi la polisi katika kurugenzi ya uchunguzi wa uhalifu Charles Twiine ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kwa njia ya simu kuwa, wasichana hao kutoka Burundi waliokolewa wakati wakiwa njiani kupelekwa nchi nyingine kwa ajili ya kufanyishwa ukahaba.

Amesema washukiwa watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kufanya biashara haramu ya kusafirisha binadamu.