NDONDI: Anthony Joshua ajipanga kummaliza Tyson Fury
2021-04-06 16:23:11| cri

Mratibu wa mapambano ya bondia Antony Joshua, Eddie Hearn, amethibitisha kuwa bondia huyo ameaanza maandalizi ya kujiandaa na pambano dhidi ya Tyson Fury, lakini pia tarehe na sehemu pambano hilo litakapo fanyika itathibitishwa wiki ijayo. Mabondia hao wawili wamesaini mkataba wa makubaliano wa kupigana ambao unaonyesha utakuwa na mapambano mawili, yenye thamani ya pauni milioni 200. Eddie Hearn amesema AJ amejipanga kwenda kuweka kambi yake ya mazoezi kwenye chuo cha michezo kilichopo mjini Sheffield, sambamba na mkufunzi wake Rob McCracken. Mratibu huyo akaweka wazi kuwa mpaka wiki ijayo mipango yote juu ya pambano hilo litafanyika wapi na lini itakuwa imekamilika.