Sudan imesisitiza kubadilisha njia ya mazungumzo kuhusu Bwawa la Grand Rianissance Rianissance (GERD) baada ya siku 200 “zisizo na ufanisi”. Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bibi Mariam Al-Mahdi amesema duru za mazungumzo yaliyofanyika chini ya usimamizi wa Umoja wa Afrika hazikuwa na ufanisi, na kusababisha kurudi nyuma kwa matokeo yaliyofikiwa katika mazungumzo ya awali.