SOKA: CAF yaja na mpango mpya vipimo Covid-19
2021-04-06 16:22:12| cri

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) linajiandaa kutoa mwongozo mpya wa usimamizi wa vipimo vya virusi vya Corona kutokana na changamoto nyingi zinazoibuka katika mashindano mbalimbali inayoyasimamia. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CAF Alexander Siewe imesema, Shirikisho hilo linaandaa utaratibu mpya wa vipimo vya COVID-19 ili kuepusha migongano na malalamiko kama ilivyotokea katika mashindano mbalimbali katika msimu huu. Hivi karibuni, kumekuwa na malalamiko ya timu mbalimbali za taifa na klabu juu ya vipimo hivyo, ambapo inadaiwa kuwa vinatumika na timu wenyeji kudhoofisha timu pinzani.