UM: Nchi zenye mapato ya chini kutopata chanjo ya COVID-9 kwa usawa ni kinyume cha maadili
2021-04-06 16:41:09| cri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, nchi zenye mapato ya kati na chini kutoweza kupata chanjo ya COVID-9 kwa usawa ni jambo linalokwenda kinyume cha maadili.

Bw. Guterres amesema, janga la COVID-19 limeonesha zaidi ukosefu wa usawa katika jamii, na kuongeza kuwa watu huambukizwa na kufariki zaidi katika jamii maskini, na zile zinazokabiliwa na hali mbaya ya maisha na kazi na ubaguzi.

Bw. Guterres pia amesisitiza, mchakato wa utekelezaji wa sera na kugawanya rasilimali wa nchi mbalimbali unapaswa kuwawezesha watu wote kupata uhakikisho wenye usawa wa afya. Jambo hilo linahusiana na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030, ambalo pia ni muhimu katika kutimiza huduma ya afya ya umma.