Russia yazuia shambulizi la kigaidi
2021-04-06 09:13:55| cri

 

Habari zilizotolewa na tovuti ya Idara ya Usalama wa Taifa ya Russia zinasema, maafisa wa kutekeleza sheria wa nchi hiyo wamezuia shambulizi la kigaidi katika sehemu ya Stavropol mpakani mwa nchi hiyo. Maafisa hao wamemkamata mshukiwa mmoja ambaye alijaribu kushambulia mamlaka ya sheria kwa bomu alilotengeneza mwenyewe, pamoja na Warussia watatu walioshirikiana naye, ambao wanashukiwa kutafuta fedha kwa makundi ya kigaidi nchini Syria, na kuliunga mkono kundi la IS.