Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Japan wazungumza kwa njia ya simu
2021-04-06 09:13:29| cri

 

 

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Japan Bw. Toshimitsu Motegi, na kusema China na Japan zinapaswa kuheshimiana, kuaminiana na kushirikiana, ili kutoa mchango kwa ajili ya amani na maendeleo ya kikanda na kimataifa. Bw. Wang ameitaka Japan iyachukulie maendeleo ya China kwa msimamo sahihi na wenye haki, na kutopotoshwa na baadhi ya nchi zinazoibagua China. Bw. Motegi amesema Japan inatilia maanani uhusiano wake na China na kupenda kudumisha ushirkiano na China.