SOKA: Ratiba ya FA Cup yasogezwa mbele
2021-04-06 16:23:31| cri

Kaimu katibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar ZFF Kibabu Haji Hassan amesema kuwa Shirikisho hilo limesitisha michuano ya Kombe la Shirikisho na mashindano hayo yataendelea utakapomalizika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Pia Kaimu katibu huyo amesema baada ya mfungo wa mwezi Ramadhan kumalizika, wataendeleza mashindano ya CONIFA ili kutoa wachezaji watakaounda kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes kitakachoshiriki michuano hiyo. Michuano ya Kombe la Shirikisho ilikuwa inatarajiwa kuanza rasmi Aprili 7,2021 ikiwa ni hatua ya 16 bora ambapo kwa sasa ligi itakayochezwa ni Ligi Daraja la kwanza na Ligi Kuu ya Zanzibar.